Steven Kanumba

Tumesikia mengi sana kuhusu kampuni ya utengenezaji filamu ya mwigizaji Mtanzania marehemu Steven Kanumba ambaye ni miaka minne sasa toka afariki.

Yaliandikwa mengi kwamba kampuni hiyo imefilisika na kwamba mama yake amelazimika kuuza vifaa vyote ikiwemo gari pamoja vifaa vingine na hii ni kutokana na kushindwa kuiendesha.
 
Kutana na wasanii wengine kwenye Bongowood kwa kuitazama bongomovie Jamal, Alhamisi saa 23:00 kwenye Maisha Magic Bongo.
 
DStv kupitia ripota Millard Ayo imempata kwenye exclusive na akasema, "Kampuni ya Kanumba haijafa, kilichotokea ni kuihamisha kwenye ofisi alipokua amepanga na kuileta nyumbani maana kodi zilizidi pale nikashindwa kumudu."
 
Mama Kanumba akaongezea, "'Kitu kingine, Kanumba ndio alikua nguzo, yaani ile kampuni yeye ndio aliifungua na ndio alijua anataka nini na maono yalikua yake, amefariki na ndio kama nguzo imeanguka maana hata mimi nikiiendesha sitoweza kufika kama yeye."
 
Kwa kumalizia Mama Kanumba amesema, "Nawaambia Watanzania kampuni bado ipo ila ipo nyumbani na kuna movie moja tumefanya na itatoka hivi karibuni... naomba tu ushirikiano wa wasanii wengine."