Mwigizaji wa bongo movie Kajala

Mwigizaji Kajala alipigwa chupa akiwa nightclub na mwanaume ambaye hamjui.

Mwigizaji Kajala amethibitisha kwamba ni kweli amepigwa chupa akiwa night club na mwanaume ambaye hamjui.

Tukio lilitokea New Maisha Club 10 May wakati alipokwenda kwenye show ya kumsaidia msanii Mabeste kuchangisha pesa kwa ajili ya matibabu ya mke wake.

Ungana na waigizaji wengine kwenye filamu ya Trinita 15 May saa 19:00 CAT kwenye Maisha Magic Swahili. Pia, burudika na filamu unazozipenda kila wakati kwa kudownload app ya DStv Now kwa simu yako ya iOS na Android.

Kajala amesema anaendelea kufuatilia hiyo ishu yake kwa polisi kwani mwanaume huyo alikamatwa na kupelekwa kwenye kituo cha Polisi cha Osterbay usiku huo huo.

Anasema haamini kama kweli mwanaume huyo alikua amelewa kama alivyosema mwenyewe manake kama angekua amelewa kweli asingeweza kuomba asamehewe dakika 60 tu baada ya kufikishwa kwa polisi.

Chupa aliyopigwa usoni imemuumiza juu kidogo ya jicho la kushoto na amefunikwa na plasta baada ya kupelekwa Hospitali Mwananyamala.