Mwigizaji Kajala

Kajala afafanua mengi kuhusu habari kuwa anadaiwa 13 million.

Kwa siku ya sita sasa stori zimekua zikichomoza kutoka kwenye vyanzo tofauti vya habari kama mitandao na baadhi ya magazeti kwamba mwigizaji Kajala anadaiwa.

Kilichoandikwa ni kwamba mwigizaji Kajala anadaiwa na anatakiwa kurudisha zile 13 milioni zilizotolewa kwa ajili yake kwenye dhamana ili kumuokoa kwenda jela, ikiwa ni pesa ambazo siku hiyo zilitolewa na Wema Sepetu.

Ungana na waigizaji wengine kwenye filamu ya Trinita 15 May saa 19:00 CAT kwenye Maisha Magic Swahili.

Kajala alipoongea na dstv.com ameyasema haya, "Aliyenilipia zile pesa hajawahi kuniambia chochote kuhusu kumrudishia hizo pesa, ni watu tu wananiandama kwenye mitandao na hii ni baada ya kuona nimeenda kweye white party."

"Wameandika Kajala unadaiwa milioni 13 zipeleke Dar Free Market chumba namba 37 inabidi uiache hela hapo, sijui wanamamlaka gani ya kuniambia nizirudishe hizo pesa wakati sio wenye nazo," alisema Kajala.

Mwigizaji huyu mwenye movie mpya ya Pishu kwenye soko la bongo movie sasa hivi amesema amekua akiandamwa kila anapotoka kwenda kula goodtime. Anasisitiza, "Mimi sijawahi kukataa kwamba sikulipiwa milioni 13 lakini haimaanishi kwamba ndio niwe najifungia ndani, yani nisienjoy maisha? haya ni maisha tu leo mimi kesho wewe."

Usisahau kuburudika na filamu unazozipenda kila wakati kwa kudownload app ya DStv Now kwa simu yako ya iOS na Android.