Msanii Juma Jux kutoka Tanzania

Juma Jux ni miongoni mwa wasanii wa RnB kutoka Tanzania akichuana vilivyo na Ben Pol na anafanya vizuri kwenye game sasa hivi na ngoma yake Wivu.

Burudika na hit hii ya Wivu kwenye Mzooka ndani ya Maisha Magic Bongo Jumatatu hadi Ijumaa saa 16:00.
 
Hit maker huyo wa Wivu amefunguka kuhusu swala la matimu kwenye game ya bongofleva Tanzania sasa hivi na kusema haya, "Muziki wetu sometimes unakuwa unalala sana, unatakiwa uchangamke. Unajua kunapokuwa na timu hata msanii unayekuwa unashindana naye kazi zinakuwa zinafanyika kwa ubora mtu anakuwa hakuchukulii poa."
 
 
Aliendelea kusema, "Lakini kitu ambacho sikipendi kwenye hizo timu zisifikie hatua zikaanza kushikana mashati, kuchomana mavisu sijui nini,” amesema.
 
'Mimi mwenyewe na Ben Pol ni wapinzani wakubwa tu, lakini tukitoka kwenye stage au studio ni washkaji lakini kikazi akitoa video ananiambia kaka nimeshakunyoosha na mimi namuambia utaona,” alimalizia.