Msanii Juma Jux kutoka Tanzania

Kutana tena na mkali wa RnB kutokea bongoflevani mkimfahamu kama Juma Jux na leo ametoa majibu ufafanuzi kwa nini Diamond Platnumz hajawahi kupost kazi kwenye social media zake haswa Instagram kama kuonesha support kama ilivyo kwa wasanii wengine.

Usikose lolote ndani ya DStv.com. Je, Diamond kamsaliti Zari? Pata uhondo yote hapa.

Kutana na wasanii hawa kutoka Tanzania Jux na Diamond kwenye na mziki yao fresh kwenye Mzooka ndani ya Maisha Magic Bongo (160), Jumatatu hadi Ijumaa saa 16:00.
 
Nanukuu maneno ya Jux, "Kiukweli niongee ukweli ni kwamba sijawahi kumtumia cover ya wimbo wangu wala yeye hajawahi kunitumia cover ya wimbo wake mimi uwa nina list ya watu kadhaa kwenye simu yangu kuna baadhi ya wasanii ambao nipo nao karibu ninawatumia kwa hiyo Diamond sijawahi kumtumia na kulalamika kwamba apost kazi zangu."
 
Jux aliendelea, "'Mara ngapi umeona post moja inajirudi zaidi ya mara 10 au  mara 20 yaani sio vitu ambavyo fulani ajakupost  basi ndio ukasirike."
 
Jux alifunga na haya, "Naomba kusema sijawahi kufanya hivyo na kwa upande wangu mtu anapostahili kupostiwa basi nitampost kwani huyo mtu anahitaji kupewa pongezi kafanya kitu fulani."
 
Mbali na Diamond, Jux ana maoni gani kuhusu matimu ya muziki Tanzania haswa kwenye bongofleva? Soma aliyosema hapa.