Msanii Juma Nature

Staa wa bongofleva mwenye umri mrefu ndani ya muziki huu Juma Nature amesema hana noma na sio ishu yeye kufanya tena kazi na P Funk Majani producer ambaye alimtoa.

Nature amemwambia ripota wa DStv, Millard Ayo kwamba katika project zake zijazo pia anaangalia uwezekano wa kupata mikono ya jajani kwenye beat zake ili kuendeleza kazi nzuri kwenye chat ya bongofleva.
 
Nature ambaye sasa hivi ana single mpya ya Kidaruso ft. Cannibal amesema P Funk hajawahi kukosea toka ameanza kufanya nae kazi, na hata mpaka leo album ya Ugali ndio album yake iliyompa mafaniko makubwa sana.
 
Pata kutazama Juma Nature na Bongo staas wengine kwenye Mzooka kwenye Maisha Magic Bongo (160), Jumatatu hadi Ijumaa saa 16:00.
 
Nature amesema kilichofanya asifanye ngoma nyingi na P Funk kwa miaka ya karibuni ni sababu ya studio yake. Nature anamiliki studio yake ambayo kaajiri Producer ambaye huusika kutengeneza nyimbo za wasanii wapya na za Nature pia.
 
Kwa kumalizia pia Nature amezungumzia uhusiano wake na Chege sasa hivi na kusema hakujawahi kuwa na beef ya ugomvi kati yao na kwamba kilichokuwepo ni ushindani wa kimuziki tu so wako poa sasa hivi na hata ngoma wanaweza kufanya.