Vincent Kigosi kwenye Maisha Magic Bongo

Maisha Magic Bongo inakutuza kwa kuwa mtazamaji wetu bora mwezi huu na filamu mpya na za kipekee sana katika mwezi huu wa Julai. Na tuangale yapi waliotuandalia.

Director Zeddy King anatuletea Kiporo ambapo Mzee Mkali na hajafurahishwa na kitendo cha binti yake kuishi na mwanaume bila ndoa. Anamua kuenda kuwatembelea na anapewa  mahari ya binti yake, basi  vituko vinaanza kati yake  na mume wa binti yake  kumtaka kijakazi kwa lazima. Je nani atampata? Shuhudia haya yote Jumatano 6 Julai saa 20:00 EAT.

Hapatoshi- Mjomba anahitaji matibabu haraka sana mjini, Binaumu yake Slim anakuja kwa nia ya kumpeleka hospitali, kumbe Mjomba anamipango yake mingine inayomuweka Slim matatizoni. Tazama vile Slim anavyopata tabu na wageni wake kisa tu ni Mjomba wake. Je ni haki? Tazama siku ya Alhamisi 21 Julai saa 20:00 EAT.

 

Katika filamu Siri ya Ginigi  ungana na Salim Ahmedy, Salma Omary, Korongo Hamis. Pale Sabla anaposistiza kwenda kujifungua kijijini kwa mama yake, huku shangazi yake nae anamipango mengine juu ya mtoto wa Sabla. Lakini mume wake anafanikiwa kuokoa familia yake . Usikosee kushuhudia misukosuko ya Sabla Alhamis 7 Julai saa 20:00 EAT.

Vincent Kigosi pamoja na Blandina Chagula wanatuletea The Shell ambapo Wilboard na Dlaphina wanandoa yenye furaha. Furaha yao inaingia dosari baada ya kugundua kitu cha ajabu ndani ya nyumba yao. Je ni kitu gani kilichotokea? Ungana nasi siku ya Alhamisi 28 Julai saa 20:00 EAT kutengua kitendawili hichi.

Katika Last Decision, Adam anampeda sana  Boke lakini tamaa ya utajiri inamvaa kwa kishindo. Adam anajikuta akitafuatwa na polisi kwa sababu ya kumuokoa mtoto anayetafutwa na pia mtoto huyo ni wa Boke. Kwa mengi zaidi uskikose siku ya  Alhamisi 28 Julai saa 19:00 EAT.