Rapper kutoka Tanzania Joh Makini

Leo tunaye rapper maarufu kutoka Tanzania anayejulikana kama Joh Makini mwenye hit single ya Perfect Combo akihusisha Mnigeria Chidinma. Joh Makini ni mmoja wa wasanii kutoka Tanzania wanaohusika kwenye msimu huu wa Coke Studio Africa, wengine wao wakiwa Vanessa Mdee, Yamoto Band na Navy Kenzo.

Tuliweza kukaa naye kwenye exclusive atuelezee kuhusu hip hop ya Tanzania kwa sababu kwa mara nyingi inaonekana ni bongofleva imeenea zaidi kushinda rap. Joh Makini amesema, "Hip hop Tanzania ina mashabiki wengi tofauti na nchi zingine Afrika Mashariki kama Kenya na Tanzania."

Pia alizungumzia collabo anazotayarishia mafans wake, akiwataja band ya Kenya Sauti Sol kama wasanii anaofanya nao kazi.

Yote aliyosema rapper huyu tazama kwenye video hii hapa chini:

 

Ungana na Joh Makini kwenye kipindi ya mziki moto moto Mzooka, Jumatatu hadi Ijumaa saa 16:00 kwenye Maisha Magic Bongo (160).