Msanii Jaguar

Jaguar akanusha kuwalika kwa collabo

Staa wa muziki kutoka Kenya, Jaguar amesema kolabo yake na kundi maarufu la muziki kutoka Afrika Kusini Mafikizolo ni kolabo ambayo hajailipia pesa ili ifanyike.

Kutokana na watu wengi kuona kama makundi makubwa ya muziki Afrika ni magumu kuyafikia pale mtu anapohitaji kolabo, wengi wameambatanisha kolabo zinazotokea na malipo ya kushirikiana.
 
Kutana na Jaguar kwenye Dunda Mixx, Jumatatu hadi Ijumaa saa 17:00 kwenye Maisha Magic East.
 
Jaguar anasema, "Mafikizolo waliona kazi zangu kwa Director Godfather kule South Africa, akanipigia simu na kusema Mafikizolo wanakuulizia na mimi nikasema hata mimi pia ningependa sana kushirikiana nao na tulivyoongea wakasema wanataka kufanya kazi na mimi."
 
"Sijawahi kulipa pesa msanii ili ndio anikubalie kolabo, sitofanya hicho kitu hata siku moja na ambaye atataka kunifanyia hivyo hatokuwa rafiki yangu milele," akaongezea Jaguar.
 
Ngoma mpya ya Jaguar na Mafikizolo inaitwa Going Nowhere na sasa ni miongoni mwa nyimbo ambazo utaziona sana kwenye TV zako kama MTV Base na TRACE Urban ambazo zote ni channel zinazopatikana kwenye DStv.