Msanii anaefanya vizuri kwenye game ya muziki Afrika pia ni miongoni mwa wasanii bora nchini Nigeria namzungumzia Iyanya ambae amefanya hit single nyingi na nzuri kama Mr.Oreo, Applaudise, Nakupenda( ft Diamond Platnumz) pamoja na hit zengine.

Iyanya amezikamata headlines baada ya kuripotiwa kuwa ameiacha manangement yake ya zamani na kwa sasa amesainiwa chini ya label ya producer maarufu wa Nigeria Don Jazzy.

Iyanya ameeleza kuwa kweli yeye ni Mavins kutokana na kusainiwa kwenye label hiyo ya Mavins Records yenye wasanii kama Tiwa Savage, Korede Bello, Di, Ja, Reekado Banks n.k

Iyanya ameeleza pia sababu kwanini amechagua kuwa Mavins records kwa sasa na kuacha na Temple Manangement alikuwa aesainiwa hapo awali na haya ndio aliyoyaongea.....

“Nilikuwa nahitaji kufanya kazi na mtu ambae anaelewa music industry kiujumla na anaweza akansaidiakufikiandoto zangu katika kuufikisha muziki mahala pake na ndomana nkaamua kuingia kwa Don Jazzy, na tayari nimeshatoa single 'Up to sumting' ndani ya label hii ya Mavins” 

Kutana na wasanii wa Bongo kwenye show ya Mzooka ndani ya Maisha Magic Bongo, Jumatatu hadi Ijumaa saa 16:00.