Mwigizaji wa Tanzania Irene Uwoya

Dstv ilipopata nafasi ya kuzungumza naye kuhusu kuingia kwake kwa siasa.

Ni mwigizaji kutoka Tanzania anaetajwa kuwa kwenye list ya waigizaji watano bora wenye uwezo wa kuigiza kwenye uhalisia zaidi.

Irene Uwoya ameamua kuchukua upande wa pili na kuingia kwenye siasa akigombea Ubunge wa viti maalum Tabora na ameweza kufikia kwenye hatua nzuri.
 
Ungana na mwigizaji huyu kwenye bongo movie DJ Ben, akihusiana pia na Wema Sepetu, Jumanne 15 September saa 20:00 kwenye Maisha Magic East.
 
Dstv ilipopata nafasi ya kuzungumza nae alisema amefurahi sana kuona ndoto zake zinatimia kuwatumikia wananchi kwa upande wa siasa na ipo siku atazungumza mambo mengi zaidi.
 
Irene amefanya maamuzi ya kuingia kwenye siasa ikiwa ni miezi kadhaa tu imepita toka atangaze kusaidia watoto na shule mbalimbali kwa vitabu na vitu vingine muhimu kwa shule akisisitiza kwamba amekua akipenda pia sana kusaidia watoto.
 
Mwigizaji huyu alitangaza mpango wa kusambaza penseli, madaftari na vifaa vingine vya shule vilivyotengenezwa kwa jina lake.
 
Kwenye upande wa uigizaji kazi ambayo sio rahisi kuiacha, Irene anasema anaishukuru sanaa imemfikisha mbali mpaka kuonekana kwenye filamu kwenye Africa Magic wakati huo na waigizaji kama Ray na JB ambao ndio waliona kipaji chake na kumpa nafasi.
 
Mwanasiasa huyu anasema movie ya Oprah ambayo aliigiza na kina marehemu Kanumba na Ray kama msichana wa kisasa anayevaa mavazi fupi, ndio movie ambayo ilimpa wakati mgumu mpaka baadhi ya wazazi kumlalamikia kwamba anaharibu watoto na wanataka kuvaa kama yeye lakini anasisitiza alifanya hivyo kufikisha ujumbe.
 
Ukitaka kupata stori za mastaa unaowajua kwa inbox yako, jisajili kwa DStv newsletter utakayoipata kila wiki.