Msanii wa bongo Msami

Kwenye exclusive na DStv, Msami atoa maoni yake kuhusu skendo ati Irene Uwoya anamboost.

Tunayo nafasi ya kufahamu mengine ambayo hatujawahi kuyasikia ila kupitia hii exclusive na DStv.com msanii wa bongofleva na dancer, Msami amekubali kuongea ya moyoni.

Wengi wanaona kama skendo ya kutoka kimapenzi na Irene Uwoya ndio imemnyanyua na kufanya awe maarufu ila yeye anachojibu ni hiki, "Siamini kwenye hilo, mimi binafsi sipendi skendo, inanibo kuona watu wanaamini hii."

Msami aendelea kusema, "Irene atasimama kama Irene, mimi ni dancer pia ila sijawahi kucheza na Irene au kutaja jina la Irene kwenye stage, nafanya kazi yangu tu isitoshe yule ni mke wa mtu so naheshimu hilo."

Mengi kuhusu mambo ya ndoa na maisha ya kinyumbani, kutana na Bi Mariam Wamigambo akikupa mawaidha kem kem kuhusu pia ubinafsi, tabia njema na desturi za wanawake kwenye Mchichiko wa Pwani saa 19:00 EAT kwenye Maisha Magic Bongo.

Kwenye sentensi nyingine, Msami amesema, "Kazi yangu ndio inaniboost, nimekwenda nchi nyingi ikiwemo Marekani na Netherlands, huko kote wameniita kwa boost ya Irene? Hapana....skendo hazifanyi na sitoziruhusu kufanya kazi kwangu."

Msami yuko kwenye radio sasa hivi na single yake mpya ya Mabawa na inayo staili mpya ya kucheza.