Idris Sultan wa Tanzania

Leo tunae mshindi wa Big Brother 2014, mchekeshaji na mtangazaji wa radio, kutoka Tanzania, Idris Sultan ambaye ameelezea jinsi alivyolipokea swala la yeye kuhost tuzo za MTV Africa Music Awards sitazotolewa 22 October 2016 Afrika Kusini.

Comedian Idris Sultan ambae baada ya kupata ushindi kwenye Big Brother Afrika, ameweza kuonesha vipaji vyake mbali mbali kama uchekeshaji na utangazaji ambao anavifanya kwa sasa.

Kwenye hii exclusive na DStv.com, Idris amesema, "Kusema kweli nimefurahi kwanza kuchaguliwa kuhost kwenye tukio hili la utoaji wa tuzo za MAMAs 2016 kwa sababu nkiangalia ni moja kati ya tuzo kubwa sana afrika nzima."

Idris aliendelea kusema, "Pia ni tuzo kubwa sio kwa Afrika tu hata duniani cause zitakuwa zinangaliwa dunia nzima so watu wakubwa kama ni wanamziki wakubwa ama ni actors au directors wanangalia ni watu gani wanaweza kufanya nao kazi ndani ya Afrika so pale inamaana naenda kujiuza mimi as an artist."

Idris pia akaongezea, "Mimi ni mtu ambae napanga kuingia Hollywood na vitu kama hivyo, so nikaja kuona wamenipost na wameachwa watu vichwa kweli lakini nashukuru ni wengi sana wameweza kushow up nakusema kuwa wanataka kuniona mimi kwenye MAMAs 2016, naweza nkasema nawapenda sana mashabiki zangu na asanteni sana kwa support yenu."

Wewe kama shabiki usikose MAMAs 2016 kwenye MTV Base (322) siku ya Jumamosi 22 October saa 21:00 CAT moja kwa moja ndani ya DStv. Tayari una dekoda yako ya DStv? Basi jaza fomu hii na tutakupigia simu ndani ya masaa 48 upate dekoda kwa urahisi: