idris

Mtanzania Idris Sultan ambaye ni mshindi wa shindano la Big Brother Africa 2014 ameisogelea mic ya DStv.com na kuyaongea yafuatayo kuhusu show yake aliyoifanya Kenya kama mchekeshaji.

Idris amesema “Kwenye stand-up comedy niliyoifanya Kenya mapokezi yalikua mazuri kusema ukweli ila naweza kusema mimi ndio niliwaangusha kimtindo sababu sikuweza kumalizia vichekesho vyangu kama nilivyopanga”

'Walikua na matarajio makubwa sana kutoka kwangu kuliko nilichowapa, nimeamua kujipanga sana sasa hivi ili nikirudi tena wakati ujao nisiwaangushe' - Idris

Mshindi huyu wa BBA alihuzunishwa na kushindwa kuendelea kumalizia show yake ya kichekesho kwenye hiyo show ya Stand Up Comedy Kenya baada ya kuona watu hawacheki kama alivyotarajia, aliwaza kutofanya comedy tena lakini baada akapata moyo kwamba anaweza kukaza zaidi kwenye show zijazo.

Wapenda vichekesho? Tazama Don’t Mess with Kansiime Jumatano saa at 19:30 kwenye Maisha Magic East.

Idris ambaye alitangaza kujihusisha na biashara ya madini huku mtaji wake ukitokea kwenye ile pesa aliyoshinda BBA, amesema sasa hivi pia sehemu ya mipango yake ni kuanza kucheza filamu fupifupi za kuweka kwenye mitandao kama Youtube.