Msanii wa bongofleva Hussein Machozi

Hussein Machozi afafanua zaidi kuhusu headlines kuwa alifukuzwa Kenya

Mwimbaji wa bongofleva Hussein Machozi mwaka 2014 aliingia kwenye headlines baada ya taarifa kutoka kwamba amepewa saa 24 za kuihama Kenya baada ya kudaiwa kufumaniwa na mke wa Mwanasiasa Mombasa.

Magazeti mpaka ya Tanzania yaliandika kuhusu hizo saa 24 alizopewa Hussein ambapo baadae mwenyewe alikanusha na kusema kilichoandikwa ni tofauti na ukweli wenyewe.

Pata habari zingine za mastaa wa Kiafrika kwa kutazama Star Gist, weekdays saa 21:00 CAT kwenye AfricaMagic Showcase (DStv Channel 151).

Kwenye exclusive interview na dstv.com, Hussein leo ambaye alirudi Tanzania amesema hana uwoga wowote wa kuishi Kenya na kwamba anarudi kwenye siku kadhaa zijazo kuendelea na masomo.

Amesema ni kweli kwenye hilo tukio alikwenda kuonana na huyo mke wa Mwanasiasa lakini haikuwa chumbani, walikua kwenye swimming pool na hawakuwa kimahaba, walikutana kibiashara tu ila akashangaa habari zilizoandikwa zikapotoshwa.

Hata hivyo amekanusha kwamba alipewa saa 24 kuondoka kwenye nchi hiyo, anasema hata hizo taarifa zilizotoka aliendelea kuishi Kenya na alirudi Tanzania kwa maamuzi yake na sio kwamba alifukuzwa.

 Hussein Machozi sasa hivi ana new single kwenye TV inaitwa Ulikua Wapi.