Msanii wa bongofleva Hussein Machozi

Je, Hussein Machozi anaweza cheza soka kihodari kama anavyoimba?

Hussein Machozi ni mmoja wa watu ambao watakumbukwa kwenye bongofleva kutokana na kufanikiwa kuingia kwenye list ndefu ya hits za bongofleva toka kitambo.

Lakini kabla hatujamjua kwenye bongofleva kumbe mkali huyu alikua mzuri pia kwenye soka, yani anakipaji cha kucheza soka na alishafanya hivyo.

Kupata mengine kwenye ulimwengu wa soka, usikose kutazama shindano la Copa America kwenye SuperSport, ambapo Messi atamenyana na Neymar.

Kikubwa ambacho kilifanya aachane na soka ni kocha wake ambaye kwa sasa ni marehemu, anasema kocha huyo hakukubali kipaji chake hivyo alikuwa anamweka benchi tu.

Kwenye exclusive interview na dstv.com, Hussein amesema huenda msimu ujao akajiunga na moja ya timu kubwa za ligi kuu na akaanza kucheza soka kama ilivyokua zamani.

Anasema, "Nimeamua kulitazama soka pia labda linaweza kunitoa, naona kabisa bado kipaji changu kinaweza kutumika na nikafanya mabadiliko."

Hakikisha umejiupgrade na kifurushi cha Premium ili uweze kupata aina yote ya mchezo kwa njia ya SuperSport.