Huddah Monroe

Huddah asema yale ambayo hutaona kwenye Instagram yake.

Kwenye mfululizo wa zile stori za dstv.com leo ninae Mrembo Huddah Monroe, Mkenya aliyewahi kuiwakilisha nchi yake kwenye mashindano ya Big Brother Africa na hapo ndio akapata umaarufu zaidi.

Kwenye exclusive interview, Huddah ametaja baadhi ya vitu ambavyo hutamuona anapost kwenye page yake ya instagram ambayo mashabiki wake wengi wako hapo na huwa wanafuatilia vitu vyake.

Anasema; "Kwenye instagram yangu mashabiki watakuwa wakiona picha za maisha yangu ya nje tu lakini hata siku moja hawatoona nyumba yangu, boyfriend wangu au maisha yangu private."

Nunua Explora yako leo, upate habari za mastaa wengine kwa HD, yaani High Definition kwenye Wendy Williams Show Jumatano saa 22:00 kwenye BET (129).

"Niliamua sitompost boyfriend wangu sababu ukimpost wanawake wanaanza kumfollow, kumtongoza na kumtumia picha zao ili wamshawishi.... sasa hiyo mimi sipendi," Huddah.

 

 

"Kitu hutaona kwenye Instagram yangu ni pale mahali nalala, ninapoishi, hata mama yangu au familia yangu sitoweza kuipost, huwa inaumiza unapompost mtu alafu anatukanwa kwenye comments," asema Huddah.