Huddah Monroe

Haya ndio maoni ya Huddah Monroe kuhusu ndoa.

Ripota wako wa nguvu Millard Ayo alikutana na staa mwingine wa Afrika Mashariki wiki hii ambaye ni Huddah Monroe, Mkenya aliyewahi kuiwakilisha nchi yake kwenye mashindano ya Big Brother Africa.

Alipoulizwa na Millard kuhusu kuolewa, Huddah alisema hadhani kama itakuja kutokea ameolewa na sababu kuu ni anayoyaona kwa marafiki zake.

Kupata habari za mastaa wengine, tazama kipindi cha E! News Jumatano saa 17:45 kwenye E! Entertainment (124).

Huddah ambaye ni mcheshi, alisema kikubwa kinachomfanya asiolewe ni yale mateso anayoyaona kwa marafiki zake walioolewa, wanaoteswa na waume zao huku ndoa zao bado ni changa.

 

 Yote haya aliyasema pamoja na kutaja sababu zilizomfanya ashindwe kuhudhuria Zari All White Party pamoja na kwamba alikuja Dar es Salaam kwa ajili hiyo weekend iliyopita.

 Amesema kilichomfanya ashindwe kuhudhuria ni kujisikia vibaya kiafya na wala hakuna tatizo lolote lililotokea, anasema 'nawaheshimu na wao wananiheshimu hivyo kusingetokea chochote kibaya, sisi ni marafiki wazuri'