Idris Sultan

Idris ameongelea hofu aliyonayo kiimani kipindi hiki cha Ramadhan

Ikiwa ni kipindi cha mwezi mtukufu wa Ramadhan, mchekeshaji maarufu Tanzania, mtangazaji wa radio na mshindi wa shindano la Big Brother Africa mwaka 2014, Idris Sultan ameeleza hofu aliyonayo katika kipindi hiki cha Ramadhan.

Mengi ya bongo, tazama Mzooka siku ya Jumatatu hadi Ijumaa saa 16:00 ndani ya Maisha Magic Bongo (160).

Idris anasema binadamu wanafanya makosa mengi na kutumaini kupata rehema za mungu katika kipindi hiki cha mwezi mtukufu kwa njia ya kufunga na kuweka ukaribu na mungu lakini yapo mengi ambayo watu wanajishau ilihali wanafunga na hiyo ni hofu yake kubwa katika kipindi hiki ambacho muislamu unapaswa kujitakasa madhambi yako.
 
Amesema, "Unajua hatupaswi hata kusikiliza muziki ila wapo wenzangu ambao ni waisilamu na ni wanamuziki mahiri kabisa, tunasikiliza na kufurahi miziki hata wakati wa swaumu na hiyo ni dhambi."
 
Idris aliongeza, "Natamani hata mwezi mtukufu ukiisha niweze kuepukana mahusiano ya kimapenzi labda mpaka nioe ila sidhani kama ni leo wala kesho hivyo naogopa hata kama swala zangu zinafika kweli."