Mtanzania Hellen Dausen kwenye jarida la Forbes

Hellen Daunsen ni mrembo wa kitanzania ambaye jina lake limetajwa sana kwenye siku za karibuni baada ya kutajwa na jarida maarufu la Forbes kwamba ni bilionea wa siku chache zijazo.

Kilichomfanya atajwe kuwa bilionea ajae ni bidhaa za asili anazozitengeneza kwa ajili ya kutumika na binadamu kama mafuta ya kupaka kwenye ngozi na kwenye nywele.
 
Mbali na Mtanzania huyu bilionea, pia kutana na mastaa wengine kutoka Tanzania kwenye Inside Bongowood, Jumanne saa 15:30 kwenye Maisha Magic Bongo
 
Swali ni: Je katika bidhaa zake amepanga kutumia sura za mastaa wa bongo ili kupata attention zaidi na kusukuma soko lake kujulikana na watu wengi zaidi kwa haraka?
 
 
Jibu ni hapana. Anasema, "Kwa kweli sijawahi kufikiria hilo swala la kutumia wasanii kwenye matangazo ya kibiashara kwenye bidhaa zangu, mimi mwenyewe ningependa kuwa sura ya brand yangu."
 
Kaongezea, "Nimekua kwenye industry ya uwanamitindo kwa muda mrefu ikiwemo kushinda Miss Universe 2010, sijawahi kuwaza msanii gani ambaye angeweza kuiwakilisha brand yangu kama ambavyo ninavyotaka, bado kwa sasa."
 
Kiwanda cha Hellen kiko Zanzibar kwa sasa na amesema hana mpango wa kukihamishia Tanzania bara sababu kuna vitu vingi anavyovipata kwa urahisi akiwa Zanzibar.
 
Pata  DStv HD decoder kwa TZS 59,000 au DStv Explora kwa TZS 185,000 kwa kujaza form hii hapa!