Msanii wa Tanzania Harmonize

Harmonize aongea kuhusu warembo anaopenda kuwaweka kwenye video zake.

Ni mwimbaji wa bongofleva ambaye anatokea WCB lebo inayomilikiwa na mwimbaji Diamond Platnumz ambapo Harmonize ni msanii wa kwanza kuanza kufanya kazi chini ya lebo hiyo.

Wakati ambapo tayari video yake mpya ya Bado imefikisha views zaidi ya milioni moja Youtube kabla hata wiki mbili hazijatimia, Harmonize ameongelea uhaba wa wasichana wa Kiafrika kwenye utengenezwaji wa video za muziki sasa hivi.

Burudika na hit single hii ya Bado kati ya Harmonize na Diamond kwenye Mzooka, Jumatatu hadi Ijumaa saa 16:00 kwenye Maisha Magic Bongo (160).

Kwenye exclusive interview na DStv, Harmonize amesema angetamani sana anapokwenda Afrika Kusini kufanya video yake aletewe video queen wenye asili ya Kiafrika kwa asilimia 100 na sio hawa wenye mchanganyiko.

Ni kitu ambacho hata yeye amekua akikitamani sana na aliwaza kuchukua Watanzania aende nao South Africa ni gharama sana sababu ya nauli, malazi na chakula.

Amekiri kwamba video vixens huwa wanaletwa kwa wasanii wawachague wenyewe na inakuta wengi ni kama wenye asili ya kizungu na sio Kiafrika kwa asilimia 100, na pia wenye asili ya Afrika huwa ni wachache sana na inakuta hawajafikia sifa za kuwa kwenye video yake ila ni kitu angetamani sana kufanya video na warembo wenye asili ya kiafrika kabisa.

Harmonize pia unaweza kumsikiliza wakati wowote unaporekodi nyimbo zake na Explora yako ama kumchezesha tena na tano. Jaza fomu hii kupata Explora au pia HD decoder kwa urahisi: