Msanii wa bongofleva H Baba

H Baba amethibitisha amerudi nyumbani Mwanza na alikua akifanya mazoezi na club hiyo na kwamba mashabiki watarajie anaweza kuonekana ligi kuu msimu mpya.

Tunae msanii wa bongofleva H Baba kwenye hii page ambaye ameingia kwenye headlines za kuuacha muziki na kuhamia kwenye soka chini ya club ya Toto African ya Mwanza.

Kwenye exclusive interview na dstv.com, H Baba amethibitisha amerudi nyumbani Mwanza na alikua akifanya mazoezi na club hiyo na kwamba mashabiki watarajie anaweza kuonekana ligi kuu msimu mpya.

Mengi zaidi kwenye soka, usikose kutazama CECAFA Kagame Cup itakayopeperushwa live kwenye SuperSport kutoka mjini Dar es Salaam, tarehe 18 July - 2 August.

H Baba amesema yeye amekua akicheza soka toka kitambo sana sema alirudi na kuegemea sana kwenye muziki na filamu lakini kiukweli soka analo kwenye damu na hakuna hata kimoja kati ya hivyo atakiacha, soka muziki na filamu kote ataenda navyo sawa.

 

 

Dstv.com haikuishia kwake tu, iliutafuta uongozi wa club hiyo ambao kweli ulithibitisha H Baba anafanya mazoezi na timu hiyo ila hajasajiliwa bado lakini akionyesha kiwango kizuri kwenye mazoezi basi watamchukua.

Endelea kukaa karibu na dstv.com ili kila stori inayonifikia ikufikie na wewe pia hasahasa hii ya H Baba ambaye bado tunaendelea kufatilia kujua itaishia wapi.

Usikose kuitazama CECAFA Kagame Cup kwenye SuperSport.