Msanii kutoka Tanzania Grace Matata

Leo tunaye mkali wa sauti kutoka Tanzania Grace Matata ambapo imebidi post hii itumike kufahamu kuhusu ukimya wake kwenye muziki pamoja na kuamua kujikita zaidi kwenye muziki wa live na sio tena bongofleva kama mwanzoni.

Grace kaacha bongofleva lakini wasanii wengine wa bongofleva bado unaweza ungana nao kwenye Mzooka, Jumatatu hadi Ijumaa saa 16:00 ndani ya Maisha Magic Bongo (160).

Kama ulianza kumsahau, mkali huyu ndio mmiliki wa hit single Free Soul iliyofanya vizuri na badae kuachia album yake Nyakati na hapo akawa kimya kwenye bongofleva na kujikita zaidi kwenye muziki wa live band.

Kwenye exclusive na DStv ametoa sababu za kufanya live music, "Nilikuwa napenda zaidi live Music toka naanza muziki na nikaona pia kama mwanamuziki unatakiwa uwe na njia za nyingi za kujiexpress."

Grace Matata aliendelea kusema pia hata role models wake walikuwa wote ni live perfomers. Mwanadada huyu alimalizia, "In time unatakiwa uwe na njia tofauti za kujingizia kipato kama msanii lakini pia naona ukiwa kama recording artist tu sio perfoming artist inakuzua sana, and muulize mtu yeyote utaambiwa live music is the best."