Msanii wa Tanzania Godzillah

Tunaye rapper kutoka Salasala Dar es Salaam ambaye ni mmoja waliopewa nishani za kuwa wakali wa ku-freestyle, Godzillah.

Ukimuuliza ni kitu gani kinachomiss kwenye bongofleva atakwambia kikubwa kwake ni upendo, anaamini upendo umekosekana kwa kiasi kikubwa miongoni mwa wasanii wa bongofleva.
 
Lakini wanacho wasanii hawa ni nyimbo motot motot. Ungana na Godzillah na wenzake kutoka Tanzania kwenye Mzooka Jumatatu hadi Ijumaa saa 16:00 kwenye Maisha Magic Bongo.
 
"Ni rahisi mtu kukuchekea usoni lakini kiukweli ndani ya moyo ana yake, tunatakiwa kuurudisha upendo... tufanye kazi tupeane support, hiyo itatufikisha."
 
Kwenye upande mwingine Zillah ameonyesha wazi kutokua tayari kuzungumzia beef au headlines zilizoandikwa na yeye kutopatana na msanii mwenzake aitwae Billnas.
 
Kingzilla amesema anachotaka ni kwamba muziki mzuri na support ndio vitangulie kwenye headlines, mengine yote ambayo hayana msingi yaachwe sababu hakuna umuhimu wa kuyabeba.