King Crazy GK posing for the camera.

Msanii GK hawasifu wasanii wenzake wa Afrika Mashariki kama Diamond Platnumz, Ali Kiba, Ommy Dimpoz na Vanessa Mdee.

Bongofleva ambayo inayo list ndefu ya wakali waliowahi kuingia kwenye headlines, itamkumbuka hata King Crazy GK kutoka East Coast Team.

Kwenye exclusive interview na DStv.com, King GK amesema anajivunia sana kuwa na Diamond Platnumz kwenye bongofleva.

Namnukuu akisema: "Hauwezi kwenda Nigeria ukafanikiwa kwa kuimba muziki kama Wanigeria, watakushangaa kwanza na hutakua na kipya lakini kwa aina hiihii ya muziki wetu lazima wakukubali sababu una kitu tofauti."

Wasanii wengine aliowasifia GK ni pamoja na Ommy Dimpoz na Vanessa Mdee kwa kusema wakali hawa nao wameweza kuiwakilisha Tanzania vizuri, wanafanya kazi nzuri sana kupitia muziki wao hata nje ya mipaka.

Ameisifia pia single mpya ya Ali Kiba Chekecha kwa kusema ile ni mikono tofauti kabisa, hata ukiipeleka kwa Wasouth Africa na Nigeria lazima waisikilize na kuipenda sababu ni kitu tofauti na wanachokifanya kwenye muziki wao.

Kuwacheck mastaa wengine wakiafrika tazama kipindi cha African Stars, Mondays saa 17:00 CAT kwenye SuperSport 9 (209).