Msanii Akothee wa Kenya

Kwenye DStv.com leo tuna mwanadada kutoka Kenya Akothee anaefanya vizuri kwenye game ya muziki kwa Afrika Mashariki akiwa miongoni mwa wanadada bora na tayari anatuzo mbili.

Tunafahamu kuwa mrembo huyu ambaye ameshafanya kazi na msanii kutoka Tanzania Diamond Platnumz iliobebea jina la My Sweet Love kwa miezi iliopita na kwa sasa anatamba na wimbo wake Yuko Moyoni.
 
Burudika na ngoma ya Akothee kwenye Kenya 10 saa 20:00 ndani ya TRACE Mziki (323).
 
Kwenye post hii Akothee ameeleeza wazi kwa watu kiwango halisi ambacho yeye anaweza kufanya nacho collabo na msanii mwingine yeyote yule, na hiki ndicho kiasi alichotaja  na ameleza wazi kuwa bila msanii kuwa nacho hawezi fanya collabo.
 
 
Akothee amesema, "Kama msanii hautakiwi kukimbilia kusainiwa chini ya record lebels, unaweza pata pesa kutokana na social media zako, usijikalishe na kusubiri pesa zije. Sasa kwa upande wangu wala usijisumbue kunipigia simu kama hauna shilingi million moja ya kufanya collabo."