Msanii Aslay na Mkubwa Fella

Aslay alipata zawadi kubwa kutoka boss wake Mkubwa Fella

Mwimbaji ambaye ni kiongozi wa kundi la bongofleva Yamoto Band, Aslay Isihaka amekabidhiwa zawadi ya gari na boss wake Mkubwa Fella.

Baada ya kukabidhiwa Aslay ameandika; "Asante mungu kwa kunipa uhai na kipaji ambacho leo hii kina fanya naitwa Aslay pia nakushukuru kwa kunifikisha kwenye mikono ya mtu mwenye moyo wa kibinaadamu."

Nunua Explora yako leo, upate habari za mastaa wengine kwa picha ya High Definition kwenye E! News Jumatano saa 17:45 kwenye E! Entertainment (124).

"Najua kuna mengi makubwa ambayo boss wangu @mkubwafella umenifanyia ambayo si vyema kuyataja yote kwasababu wakati wake haujafikia ila naomba nichukue fulsa hii kukushukuru kwa hiki ulichonifanyia leo katika sherehe Ya kusherehekea siku yangu ya kuzaliwa."

"Umenifanya nijione mwenye thamani kubwa duniani sikutegemea kama leo itakuwa siku yangu ya kumbukumbu ambayo sitoweza kuisahau hata Nije kuwa bilionea @mkubwafella asante kwa kunipa hii zawadi ambayo mimi kama mimi sikuiwazia kabisa kama Leo nitapata gari."

"Ninaushukuru uongozi mziki Wa #mkubwanawanawe pamoja na manager wangu @chambusso boss wangu @babutale @mhtemba na mama yangu @sweatfella bila kuwasahau wasanii wenzangu wa @yamoto_band mungu ndie atakaewalipa."