Diamond Platnumz na Zari

Ni good news nyingine kwa msanii wa Bongofleva Diamond Platnumz ambaye Jumanne tarehe 6 December 2016 mpenzi wake Zarina Hassan amefanikiwa kujifungua mtoto wake wa pili, Zari na Diamond wamepata mtoto wao wa pili baada ya kupata mtoto wao wa kwanza Tiffah August 2015.
 
Zari amejifungua  saa 10:35 alfajiri katika hospitali ya Netcare  Pretoria South Africa lakini Diamond alipost kutumia ukurasa wake wa Instagram na kueleza furaha yake.
 
 
Na tayari wamefikia muafaka kumpa mtoto wao ina ambaye anaitwa Riaz Naseeb Abdul na amefunguliwa page instagrama kama ilivyofanywa kwa mtoto wao wa kwanza Tiffah na kuiita PrinceRiaz2016. Na tayai ndani ya siku mbili ina followers zaidi ya laki mbili ikiwa na post tano tu.
 
Pia jiunge na Diamond kwenye kipindi cha Mzooka saa 16:oo Jumatatu hadi Ijumaa ndani ya Maisha Magic Bongo.