Bongo rapper Fid Q

Fid Q kwenye list ya rapper bora Afrika

Rapper Fid Q kutoka kwenye bongo Hip-hop ameingia kwenye headlines baada ya kutajwa kwenye list ya Marapper 20 bora wa Afrika 2015.

Jiunge na marapper wengine kwenye kipindi cha Rush Hour, Ijumaa saa 18:00 kwenye MTV Base.

Baada ya hiyo good news, staa huyu wa single ya Bendera ya Chuma ambayo ipo mpaka kwenye chati kubwa ya muziki Tanzania. Fid Q amesema anaamini atafika kwenye namba 1 ya chati hiyo.

Namnukuu: "Naamini tutafika namba 1 baada ya kuachia hivi vichupa (video) ambazo zipo kwenye ratiba zinazofata, sote kwa pamoja tuseme Amen."

Single ya Bendera ya Chuma Ft. Ben Pol ina wiki 10 kwenye CloudsFM Top20 ya Tanzania na wiki iliyopita imeshika nafasi ya 13 huku kura nyingi pia zikiendelea kumwagika ipande juu.

Kwenye list hiyo ya Marapper bora 20 Afrika, wa kwanza ni A.K.A, wa pili ni Sarkodie wa Ghana na Ice Prince wa Nigeria kachukua namba tatu.

Jiunge na marapper hawa na msanii Diamond Platnumz ambaye atawakilisha Tanzania kwenye stage ya MAMAs 2015 huko Durban, Jumamosi 18 July saa 21:00 CAT kwenye MTV Base.