Msanii mkongwe kwenye bongoflevani maarufu  kama Ferooz ambaye kwasasahivi amekuwa na ukimya wa mda mrefu na ni miongoni mwa wasanii waliokuwa wakitamba na kupendwa sana miaka hiyo.

Kusikiza wimbo mpya ya Ferooz tazama kipindi cha Mzooka saa 16:00 Jumatatu hadi Ijumaa ndani ya Maisha Magic Bongo.

Ferooz baada ya ukimya mrefu wa miaka amerudi tena kivingine now ambapo zamani alikuwa na kundi liitwalo Daz Nundaz.

Kwa sasahivi Ferooz ameonesha kurudi kwenye game tena kivngine baada ya producer wake ambaye ndiye alikuwa akisimamia kundi lao la apo awali Daz Nundaz amepost kwenye ukurasa wake wa instagram kuonesha akifanya kazi mpya na kundi hilo jipya ambalo yupo Ferooz na kuweka hashtag 'Wabeshi'

Producer Majani aliandika haya kwenye ukurasa wake' Ferooz’s new group just finished recording vocals. The new Daz Nundaz and all of them are artist!! #Wabeshi.

Bila kusahau kuwa kundi hilo ambalo producer huyo nimchango mkubwa kwasasahivi chini ya Bongo Records.