MMB movie mke wa mtu

February ni mwezi wa mapenzi  na burudani ni lazima katika pilka pilka za mwezi huu. Kama kawaida Maisha Magic Bongo inawazingatia watazamaji wapendwa na filamu za kusisimua.

Mke wa Mtu Sumu- Waswahili hawakukosea waliponena mke wa mtu sumu lakini mme wa mtu maziwa. Katika filamu hii tunashuhudia jinsi wivu unaweza kusababisha maafa katika ndoa. Muhogo anafanya kila analoliweza kulipiza kisasi kwa kila mwanaume aliyethubutu kujihusisha kimapenzi na mke wake Subira. Je unahisi atatumia mbinu zipi kuwakomesha? Kweli mke wa mtu sumu. Shuhudia kisa hichi cha mapenzi Alhamisi 23 Februari saa  14:00 EAT.

Nambachi- Ni binti kutika kwa family ya kitajiri na hajakosa lolote. Lakini kama kawaida penzi ni kitovu cha uzembe kwani alijikuta akiangukia katika penzi la kijana jangili. Kama kawaidi wazazi hata kamwe hawakubaliani ma chaguo la binti wao.Kwa kweli wazazi huwa wanajua kwani walikuwa wanazuia makubwa na jambo ya kufedhehesha katika familia zao . Ni makubwa gani haya? Kwani maji yakimwagika hayazoleki. Pata kujua Zaidi Alhamisi 16 Februari saa 14:00 EAT

Jirani- Katika jamii zetu kila siku inatulazimu kuishi vizuri na majirani zetu , lakini hao hao majirani wapo wenye nia njema lakini kuna wale mioyoni mwao wamejawa  husda, wivu na chuki sisizo na mpamgilio. Katika filamu hii tegemea kuona yote haya na ni jinsi gani shukrani ya punda huwa ni mateke. Je una ushuhuda gani kuhusu jirani wako wa sasa? Tazamia kuangalia filamu hii Alhamisi 9 Februari saa 14:00 EAT.