Msanii wa Tanzania Ommy Dimpoz

Mwimbaji staa wa bongofleva Ommy Dimpoz amekaa kwenye exclusive interview na DStv Tanzania na kukubali kuongoa kwa ufupi kuhusu headlines zake zijazo ikiwemo kolabo na Mnigeria.
 
Omary Nyembo ambaye single yake ya mwisho kuachia ilikua Achia Body amesema baada ya mwezi mtukufu wa Ramadhan ataachia single yake mpya lakini hajaweka wazi kama ni kolabo na Alikiba au Mnigeria ila Watanzania wanachotakiwa kujua ni kwamba amefanya kazi na wakali wa Afrika wakiwemo wa South Africa.
 
Sote tukiingojea single hii basi kutana na Ommy Dimpoz kwenye kipindi cha Mzooka, Jumatatu hadi Ijumaa saa 16:00 kwenye Maisha Magic Bongo.