Msanii wa bongofleva Dully Sykes

Msanii wa bongofleva Dully Sykes akutana na DStv na kufafanua ni kwa nini hataki team Instagram.

Nakukutanisha na legend kwenye muziki wa bongofleva Prince Dully Sykes ambaye miaka yake ni mingi sana kwenye hit list ya bongofleva.

Kuungana na wasanii wengine wa bongo, usikose kuitazama kipindi cha Mkasi TV unayoletewa na Salama Jabir, kila Jumapili saa 19:00 kwenye Maisha Magic East.

Mtandao wa Instagram ni mtandao wa kijamii ambao umetokea kuwa na mashabiki wengi sana Tanzania hivyo wengi wanaamkia huko asubuhi mchana na mpaka usiku na kumekua na team zinatengenezwa kwa wale wenye mapenzi na watu flani.
 
Dully Sykes ametangaza rasmi hataki kutengenezewa team ya aina yoyote, anakubali mashabiki wenye upendo nae ila hataki mtu atengeneze team manake zinamtengenezea uadui na watu wengine pale team inapotumika vibaya.
 
Ameongea na dstv.com na kusema, "Sitaki kuwa huko sababu nitatengeneza maadui, hawa wanaonisuppot kila siku nitabaki nao tu ila kama wataongezeka waongezeka kwa nguvu za Mungu na sio ushabiki wa kitimu."
 
"Timu za Instagram zimeharibu hali ya hewa sasa hivi, zamani sisi kulikua kuna makundi yanashindana kwenye bongofleva lakini sio kushindana kwa ugomvi, ni kazi inapigwa alafu baadae tunatembeleana, na kulikua kuna Camp ikiwemo Misifas Camp ya kwangu, pamoja na kushindana kote lakini tulikua tunakaa tunakula na kunywa pamoja," anasema Dully Sykes.
 
Dully Sykes ni miongoni mwa mastaa wa Tanzania ambao kwenye page zao za Instagram hawamfollow mtu yeyote, mwingine kwenye hiyo list ni Ali Kiba ambapo wote wanasababu zao kwanini imekua hivyo.