Mwigizaji wa bongomovie Dude

Mwigizaji wa bongo Dude afafanua mengi kuhusu bongo Tanzania

Sio jina jipya kwenye headlines za movie Tanzania, Dude ameanza mishemishe toka time hiyo akiwa kwenye maigizo ITV na alitisha sana kwa uhodari wake kwenye kuigiza.

Sasa anaacha movie? Anairudisha bongo Dar es Salaam? Jibu lake ni hili: "Msimu mpya wa bongo Dar es Salaam ilikua kwenye maandalizi na mikakati iko palepale mpaka sasa hivi."

"Nimeamua niirudishe Bongo Dar es Salaam kutokana na soko la filamu kuyumba na wezi wa kazi za wasanii wamekua wengi, nimeamua nirudishe hiki kipindi na Watanzania wengi watakua na nafasi ya kukiona bila gharama," Dude aliendelea kusema.
 
Kutana na waigizaji wengine wa bongo kwenye bongo movie Boxeera, Jumanne 25 August saa 20:00 kwenye Maisha Magic East (158).
 
Ni kweli kuna kipindi flani serikali ilikifungia kisionyeshwe tena? Jibu lake ni hili: "Sijawahi kufungiwa ni kwasababu tu TV niliyokua nafanyia kazi haikuwa inanilipa kama ninavyotaka ndio maana nikaamua kuvunja mkataba lakini sasa hivi kuna kampuni nataka kufanya nayo na wananilipa vizuri."
 
Dude anakiri kwamba kipindi hicho akionekana kwenye TV alikua anaogopeka sana kutokana na mchezo wa wizi aliokua anaucheza hata kwenye maduka makubwa watu walikua wanamuangalia tu mpaka amalize mambo yake.

Related