Mwigizaji Dokii

Ni kwa nini Dokii amekataa kusimamia ubunge?

Mwaka 2015 ni mwaka wa uchaguzi mkuu kwa Tanzania kuchagua Rais, Wabunge na madiwani ambapo watu mbalimbali wametangaza nia ya kugombea.

Miongoni mwa waliowahi kutangaza ni Profesa Jay, mwigizaji Mzee Majuto na msanii Afande Sele lakini pia mwigizaji maarufu wa siku nyingi aitwae Dokii.

Pata habari zingine za mastaa wa Kiafrika kwa kutazama Star Gist, weekdays saa 21:00 CAT kwenye AfricaMagic Showcase (DStv Channel 151).

Dokii alitangaza kuwa na nia ya kugombea ubunge wa nyumbani kwao Morogoro zaidi ya miezi nane iliyopita lakini leo hii ametangaza habari mpya kwamba hatogombea tena.

Akiongea na dstv.com Dokii amesema ameamua kuahirisha tu na kumpisha mgombea atakaelitaka jimbo hilo, yeye atataoa support lakini hatogombea.

Amekanusha pia kwamba alitishiwa ndio maana ikawa rahisi yeye kuachana na mpango wa kugombea, amesema haya ni maamuzi yake na wala sio shinikizo la mtu yeyote.