Msanii Dogo Janja

DogoJanja ameelezea kutohitaji collabo kwa sasa ila kama ikitokea haya ndio masharti

Dogo Janja, staa wa hit singles kama My Life, Kidebe, Ukivaaje Unapendeza na nyingine kibao ameeleza kutohitaji kufanya kazi za kushirikishwa (collabo) kwa sasa mpaka hapo baadae na kusema sasa hivi ni mwendo wa hit juu ya hit anataka azidi kuaminisha watu uwezo wake.
 
Kutana na Dogo Janja na hit yake ya Ukivaaje Unapendeza kwenye Mzooka siku ya Jumatatu hadi Ijumaa saa 16:00 ndani ya Maisha Magic Bongo (160).
 
Janjaro amesema watu wengi hawachukuliii kazi serious hivyo yeye anataka kama atafanya collabo basi iwe kazi professional na sio kuunga ama kufanya kazi kishkaji hiyo imepitwa na wakati kwake.
 
Janjaro aliongeza kwa kusema watu wanajifanyia mziki bila malengo bila kujua kwamba inawaharibia wenyewe na ukishakosea kidogo tu kurekebisha ni ngumu.
 
"Unajua saivi kila mtu anataka collabo, ila yani hakuna mipango kabisa utasikia mtu anakucheki mwanangu kuna beat hapa kama inakufaa ungekuja uingize vocals baada ya hapo mnashoot video then ndo imetoka hivyo," Janja amesema.
 
Alimalizia, "Mimi siwezii hizo biashara, niite tuongee tunafanya collabo ya aina gani, tunaipromote vipi, tufanyaje ifike mbali na inawezaje kutuingizia pesa hapo sawa."