Tanzaniana artist Diamond Platnumz

Diamond Platnumz azungumzia kuteuliwa kwake kwa MAMAs na pia kushukuru mafans

Diamond Platnumz alihusika kwenye headlines za Nigeria siku kadhaa zilizopita alikokwenda kufanya media tour lakini pia kuperform kwenye Road to MAMAs ambayo inahusika kwenye tuzo za MTV Africa Music Awards 2015

Wakati tuzo zenyewe zinatolewa 18 July, Diamond amekaa kwenye exclusive interview na dstv.com na kusema ni kiasi gani tuzo za MTV zimempa nguvu baada ya kuteuliwa.

Usikose kuungana na Diamond atakapowatumbuiza kwenye stage ya MAMAs kule Durban, Jumamosi 18 July saa 21:00 CAT, ikipeperushwa live kwenye MTV Base.

Amesema ni good news kila akifikiria pale ambapo anapata mapokezi makubwa Afrika mpaka kuteuliwa kuwania tuzo zaidi ya moja kwenye MAMAs.

 

 

Kingine alichosema ni kuwashukuru mashabiki zake ambao wako na yeye na sasa wimbo wake wa Nana Ft. Mr Flavour wa Nigeria umeshika namba moja kwa wiki ya kwanza kwenye TOP 10 ya Africa kwenye TRACE Urban (DStv Channel 325).

Diamond ameahidi kuendelea kujituma zaidi ili kuhakikisha hawaangushi mashabiki zake ambao since day 1 wako na yeye.

Kuwapigia kura Diamond, Vanessa Mdee na Sauti Sol ambao pia wameteuliwa kwenye MAMAs, bonyeza hapa.