Chibu Perfume ya Diamond Platnumz

Mwimbaji staa wa bongofleva Diamond Platnumz hatimae ameiachia kwa mashabiki perfume yake ambayo alianza kuitangaza zaidi ya siku thelathini zilizopita.

Inaitwa Chibu Perfume ambapo kupitia Instagram yake alianza kwa kuwaambia watu wakutane nae kwa pamoja GSM Mall iliopo barabara ya Pugu Road DSM na kusema manukato hayo ya kwanza kutoka kwa msanii wa Tanzania ni manukato unayostahili.
 
Pia kutana na Diamond Platnumz na muziki yake kwenye Mzooka siku ya Jumatatu hadi Ijumaa saa 16:00 ndani ya Maisha Magic Bongo (160)
 
Hili ni moja kati ya mazao ambayo Diamond aliahidi kuyaleta kwa Watanzania na ametekeleza ambapo bado kuna ahadi nyingine mashabiki wanazisubiria ikiwemo headphones.
 
Soon tu atatangaza sehemu ya kuipata ambapo ahadi ya meneja wake ilikua ni kwamba watahakikisha perfume hiyo inapatikana kwa jinsia zote yaani wanaume na wanawake.