Msanii Diamond Platnumz

Diamond Platnumz avunja rekodi ya Mr Nice kwa kujaza ukumbi kule Las Vegas

Mwishoni mwa mwaka 2015 promota maarufu kwa kuandaa matamasha ya wasanii wa Afrika nchini Marekani DMK Global alikaa kwenye exclusive na DStv.com na kuweka rekodi wazi.

Moja ya rekodi alizoziweka ni kwamba rekodi ya Mr. Nice ya kujaza zaidi ya watu elfu moja kwenye show yake nchini Marekani enzi hizo yuko juu kimuziki, haikuwa kuvunjwa na msanii yeyote wa Tanzania mpaka mwishoni mwa mwaka 2015.
 
DMK leo kwenye exclusive na DStv.com amekiri kwamba rekodi hiyo imevunjwa rasmi na Diamond Platnumz kwenye show aliyoifanya huko Las Vegas Marekani ambapo zaidi ya watu 500 walikosa ticket.
 
Lakini kwenye DStv hakuna kukosa ticket, burudika na Diamond Platnumz kwenye Mzooka kwenye Maisha Magic Bongo (160), Jumatatu hadi Ijumaa saa 16:00.
 
Walikosa ticket sababu ukumbi ulijaa na mpaka polisi walilazimika kuja kusimamia kuhakikisha hakuna chochote kitakachotokea maana ukumbi ulijaa.
 
DMK anasema toka ameanza kuandaa na kuleta wasanii wa Afrika kufanya show Marekani hakuwahi kupata watu wengi hivyo Las Vegas kama alivyopata March 2016 kwa Diamond, hata Davido na P Square hawajafikia rekodi hizo.
 
Diamond pia unaweza kumsikiliza wakati wowote unaporekodi nyimbo zake na Explora yako ama kumchezesha tena na tano. Jaza fomu hii kupata Explora au pia HD decoder kwa urahisi:
 

Related