Msanii Diamond Platnumz kutoka Tanzania

2017 umeanza vizuri kwa msanii all the way from 255,Tanzania Diamond Platnumz (Simba). Good news kwako kama wewe ni shabiki wa Platnumz basi nakusogezea rekodi hii aliovunja tena msanii huyu kwa mwaka 2017.

Tovuti ya rapper maarufu wa Marekani 50 Cent inayojulikana kama thisis50.com iliyoanzishwa mwaka 2007 kwa lengo la kuendeleza kusambaza habari za utamaduni na mahadhi ya pop na hiphop. 

Uliyaskia ya Vanessa Mdee kupata dili nyingine Nigeria? Yote yapate hapa.

Mwimbaji Diamond ameingia kwenye headlines baada ya kuvunja rekodi ya kuwa msanii wa kwanza Mtanzania baada ya video yake mpya aliyomshirikisha Mmarekani Ne-Yo Marry You kuwekwa kwenye tovuti hiyo.

Wimbo huu wa Marry You sasa unaweza kuisikiliza kwenye Mziki Fresh Jumatano saa 18:00 ndani ya Trace Mziki (323).

Tovuti hiyo iliwaambia watembeleaji waitazame video mpya ya Diamond kwa kuandika:

“Angalia video mpya ya Mtanzania mshindi wa tuzo, Diamond Platnumz Marry You akishirikiana na Ne-Yo.”

Video hii imetoka siku chache tu ambayo kwa sasa hivi ina siku saba tangu iyachiwe na ndio video iliyoko kwenye nafasi ya kwanza kwenye trending videos kwenye mtandao wa Youtube.

Video hii imevunja rekodi tena kama ile ya Salome ya Diamond Platnumz ft Rayvanny ambapo Marry You tayari ilifikisha zaidi ya 1 Million viewers ndani ya siku tano tu.

Baada ya Salome, Rayvanny ametangaza collabo nyingine na Diamond Platnumz. Soma yote hapa.