Msanii Diamond Platnumz

Tunae staa wa Tanzania Diamond Platnumz anayekujia kuhusiana na skendo zote ambazo amezipata juu ya kumsaliti mama watoto wake Zari. Haya ndio yalikuwa majibu yake Diamond.

"Kitu ambacho niko proud sana ni mpenzi wangu Zari nimwelewa sana,na tangia tunaanza anaelewa kwamba mimi nimaarufu na yeye ni maarufu. Mimi nitasikia vitu kumhusu yeye na yeye atasikia vitu kunihusu, mimi ni staa naishi Tanzania ofcourse ni mtu ambaye nikiwinda siwezi kukosa au kuna mtu anaweza kuniwinda kinamna yoyote ile."
 
Diamond aliendelea, "Lakini mwisho wa siku ni ufahamu wangu mimi kuwa mwanaume na ni namna gani naweza kumheshimu mwenzangu, kuweza kumpenda mwenzangu,na kumlindia heshima yake, na najikinga vipi na hivyo vitu vibaki kuwa story na sio vitu vya kweli kwasababu kusema vitasemwa tu."
 
Akamalizia, "There is no way Simba akapita katika zizi la swala akaondoka watu wakasema hakula swala hata mmoja watasema tu alikula hata kama hakula."
 
Mengi kuhusu mapenzi, harusi na maisha ya ndoa ya Watanzania, zipate kwenye Harusi Yetu ndani ya Maisha Magic Bongo (160) kila Jumaapili saa 18:00.