Kundi la Navy Kenzo kutoka Tanzania

Baada ya mastaa wa bongofleva Navy Kenzo kupata mialiko ya kutumbuiza kwenye miji mbalimbali nchini Israel, Diamond Platnumz amenyanyuka na kuyaandika yafuatayo.

Kutana na kundi hili kutoka 255 Navy Kenzo kwenye Mzooka siku ya Jumatatu hadi Ijumaa saa 16:00 ndani ya Maisha Magic Bongo (160)

Amepost video ya sehemu ya show za Navy Kenzo na kuandika, "Kutoka Tanzania mpaka Israel... unaweza zani jambo rahisi ila sio dogo kama ufikiriavyo..hii ni hatua kubwa tena sana..and am super proud of you Navykenzo."
 
 
Navy Kenzo walialikwa kwa ajili ya kufanya show tatu lakini baadae wakaongezewa show moja hivyo kufanya jumla ya show zao kuwa nne ambapo wanaishikilia rekodi ya wasanii wa bongofleva waliotumbuiza Israel.
 
Haijawahi kutokea kabla kwa msanii wa bongofleva kualikwa Israel na kwenda kutumbuiza, ilizoeleka kwenye nchi nyingine tu kama Afrika Kusini, Marekani na nchi nyingine za Ulaya lakini kwa Israel rekodi inashikiliwa na Navykenzo kuwa wa kwanza kwenda kutumbuiza.
 
Show za Israel wameonekana mashabiki mbalimbali ambapo huu ni muendelezo wa tour ya dunia ya Navy Kenzo ambayo itakwenda kwenye nchi nyingine kama Marekani baadae mwaka huu.