Msanii Diamond Platnumz

Msanii wa bongofleva Diamond Platnumz amekuja na njia mpya ya kuendeleza biashara ya mziki wa bongo ambao pia utanufaisha wasanii pamoja na kampuni yake ya WCB kwa kufungua mtandao kwa ajili ya kuuza nyimbo.
 
Mtandao huo unaitwa Wasafi.com ambao pia utawezesha mashabiki kupakua nyimbo za wasanii wanaopenda, ambao watatumia platform hiyo kuuza nyimbo zao.
 
Burudika na hit ya Diamond akimhusisha Ne-Yo Marry You kwenye Mzooka siku ya Jumatatu hadi Ijumaa saa 16:00 ndani ya Maisha Magic Bongo (160)
 
Diamond ameeleza pia shabiki atachangia kiasi kidogo cha pesa ili kukuza uchumi wa msanii pamoja na pato la kampuni kupitia huduma hiyo.