Msanii wa bongofleva Tanzania Dayna Nyange

Ni mwimbaji wa bongofleva Dayna Nyange ndiye anahusika kwenye hii post ya DStv.com akiongelea ishu ya ngozi yake kuwa nyeupe ikiwa ni tofauti na ile aliyozaliwa nayo.

Dayna amesema kilichotokea ni kwamba alikwenda kununua mafuta kwa ajili ya kung'arisha ngozi na sio kujichubua lakini ghafla matokeo yakawa ni kubadilisha rangi ya ngozi kabisa.
 
Mbali na ishu ya rangi ya ngozi yake, kutana na mrembo huyu Dayna na muziki yake kwenye Mzooka, Jumatatu hadi Ijumaa saa 16:00 kwenye Maisha Magic Bongo.
 
Hata hivyo Dayna anasema hajutii kwa kilichotokea sababu ni mapito ya ujana na yuko wazi kuongea sababu anataka wasichana wengine pia wajifunze, yeye anasema amejikubali na hiyo hali tayari.
 
"Watoto wa kike tunataka kung'aa na kumeremeta, nilikua napaka yale mafuta kidogokidogo nikaona nang'aa nikaendelea kuzidisha kipimo ndio hapo nikapitiliza ila sio ishu, ni vitu kwenye maisha tunakumbana navyo na hatuna budi kukubaliana navyo na kuelimisha wengine," kasema Dayna.