Davido na Diamond Platnumz

David afafanua zaidi kuhusu beef yake na Diamond

Zilitoka stori toka mwaka jana mwishoni baada ya tuzo za Channel O kutolewa na mshindi wa BBA 2014 kutangazwa Mtanzania Idris.

Kuna tweet aliyotweet Davido kwamba 'they cheated again' ambayo wengi waliamini lilikua ni dongo kwa Tanzania, kwamba imeshinda tuzo 3 za Channel O na BBA 2014.

Tweet hiyo iliyoonekana kumaanisha 'wamedanganya tena' ilizua hedlines na comments za matusi zikaanza kumiminika kwa Davido na mpaka baadae ikaonekana kama kuna beef kati ya Diamond na Davido.

Kutana na wawili hawa kwenye MTV Awards Music Awards 2015 itakayopeperushwa live kutoka Durban kwenye MTV Base (322) na BET (129) Jumamosi 18 July saa 21:00.

Hata hivyo pande zote mbili zilionyesha kwamba hakuna beef baada ya kukutana Durban South Africa ambapo Diamond na Davido walipiga picha ya pamoja na kuzipost kwenye page zao.

Baadae Davido aliongea kwenye Exclusive na dstv.com na kusema hakuna beef kati yake na Diamond na kwamba Tanzania ni nyumbani kwake kwa pili.

Akamalizia kwa kusema, kilichotokea ni kutoelewana tu kwa upande wa mashabiki manake alichokiandika kilichukuliwa tofauti kabisa na alichomaanisha, anaipenda Tanzania.