Rapper Darassa kutoka Tanzania

Unaweza ukwamwita mzee wa Too Much, Darassa ni rapper ambae kwa sasa hivi anatisha na ngoma yake mpya ya Mziki akimhusisha msanii wa R'n'B kutoka Tanzania Ben Pol.

Ngoma hii mpya sasa inapatikana kwenye kipindi moto moto cha Mzooka ndani ya Maisha Magic Bongo, Jumatatu hadi Ijumaa saa 16:00. Usikose.

Darassa ameingia kwenye headlines baada ya hit song yake kufanya vizuri. Kwa sasa hivi Mziki ndio inayoongozwa kwa kusikikwa zaidi redioni nchini Tanzania na kupelekea mashabiki kumtaja kama rapper namba moja.
 
Darassa akaamua afunguke baada ya comment kutoka kwa mshabiki zake na haya ndiyo yalikuwa maneno yake.
 
"Sikuwa nimeplan hivyo lakini naona watu wanaweka huo mtazamo kwa sasa kutokana na hard work niliyo ionyesha na still nipo bado nipo kwenye changamoto ya kufanya kazi kwa bidii kuhakikisha nafikia malengo yangu. Lengo langu si kuamka asubuhi watu wakasema mimi ndio best rapper au mimi ninaweza kuwa mkali kwenye hiki kipindi lengo langu ni kuweka historia kwenye muziki wangu hata kama nisipotoa wimbo historia yangu ibaki inafanya kazi. Naomba Mungu anisaidie sana kwa hili.”
 

Aliendelea, “Nafikiri Too Much inahitaji wimbo mwingine kwa sababu toka nimeutoa hakuna wimbo mwingine unaweza kukaa juu ya wimbo huo. So hakuna sababu ya sisi kuendelea kusubiri mashabiki wetu wanahitaji burudani, ndio sababu kubwa imepelekea kuleta project hii mpya.”

Lakini sio Darassa tu anawakilisha na hit single mpya kwa sasa hivi. Yasikie ya Vanessa Mdee na maana ya hit yake mpya Cash Madame.