Msanii wa Tanzania Darassa

Sasa hivi tunakuletea mkali wa mistari kwenye game ya bongofleva rapper Darassa ambae wimbo wake ulimake headlines na kuitwa wimbo wa taifa kwa mwaka 2016 alieupa title ya Muziki huku akiwa amemshirikisha RnB singer wa Tanzania Ben Pol.

Rapper Darassa na Ben Pol na hit yao Muziki wanapatikana kwenye Mzooka siku ya Jumatatu hadi Ijumaa saa 16:00 ndani ya Maisha Magic Bongo.

Darassa amewataka mashabiki wa muziki wake kukaa mkao wa kula kwa ajili ya ujio ya albamu yake mpya na kudai kuwa itawawezesha mashabiki wake kuwa na nyimbo zake nyingi kwa pamoja.
 
Wajua rapper Darassa ana maoni gani kuhusu Diamond Platnumz? Kwa nini hapendi jina la simba? Yote yasome hapa.
 
Darassa alizungumza haya, '“Tutakuwa na albamu mwaka huu ambayo itarahisisha watu kupata muziki wote wanaouhitaji, tupo kwenye kipindi cha mabadiliko na nafanya ninachoweza kwa watu wangu.”
 
“Na deal na mtu ambae yupo tayari kupokea muziki wangu sitakuwa na comment kwa atakaenipinga. Changamoto zinanijenga badala ya kufikiria kitu chako ukanifikiria mimi kwenye kitu chako maana yake nimekuchallenge,” alimalizia Darassa.