Msanii wa bongo Harmonize

DStv yakuletea exclusive interview ya Harmonize, msanii wa kwanza kuachia single kutoka WCB ya Diamond

WCB (Wasafi Classic Baby) ni lebo ya Diamond Platnumz ambayo sasa hivi imeanza kufanya kazi kwa kuibua vipaji vipya vya Bongofleva.
 
Harmonize ni msanii wa kwanza kuachia single kutoka kwenye hiyo Project ya Diamond ambapo official single ni 'Aiyola' ambayo imeshika namba mbili kwenye nyimbo 20 bora za CloudsFM Top20 November hii.
 
Jiunge na msanii huyu mpya kwenye single yake ya Aiyola itakayochezwa kwenye Mzooka kwenye Maisha Magic Bongo (160), Jumatatu hadi Ijumaa saa 16:00, na pia kwenye Best of Spanking New kila Jumatatu hadi Jumatano saa 23:00 kwenye MTV Base (322).
 
Baada ya hayo, dstv.com imempata Harmonize kwenye exclusive interview ambayo unaweza kuitazama kwenye hii video hapa chini.
 
 
Pia Harmonize ameyataja yale matatu ambayo amefunzwa na Diamond kutoka waanze kufanya kazi pamoja.