Reekado Banks na Vanessa Mdee

Vanessa Mdee ameelezea juu ya collabo yake na Mnijeria Reekado Banks wa Mavin Records.

Mwanadada Vanessa Mdee anazidi kuipeperusha vyema bendera ya Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla kwenye upande wa burudani ambapo jitihada zake za kuutambulisha mziki wake nje ya Tanzania zinazidi kuzaa matunda.

Kutana na Vanessa Mdee kwenye Bongo 10 ya TRACE Mziki (323) inayopatikana sasa ndani ya DStv Catch Up kwenye DStv Explora yako.

DStv Catch Up ni nini? Soma hapa.

Pia pata mengi kuhusu umuhimu wa DStv Explora hapa.

Vanessa amekuwa akifanya collabo na wasanii wa nje ya Tanzania hali ambayo imepeleka jina lake kukua kwa kasi kwenye nchi kama Nigeria na South Afrika ambapo ndipo ameshirikiana na wasanii kama K.O, Dj Maphorisa, Mr Orezi, Ice Prince Zamani na Reekado Banks.

Vanessa ameelezea alivyokutana na Reekado na kufanya naye kazi.

"Kufanya kazi na Reekado Banks ilikuwa fresh kabisa, ni msanii ambaye nampenda, namuheshimu, napenda mziki wake na niliunganishwa na yeye kupitia Don Jazzy."

Vanessa aliongezea: "Alinitafuta na kuniomba kutia verse kwenye wimbo wao so nilipokwenda Nigeria mwaka jana mwanzoni nilitia verse yangu na tulishoot video kabisa ila haikutoka kama tulivyokuwa tunataka so nilipoenda Nigeria mwezi uliopita tukashoot video nyingine."