Vanessa Mdee kutoka Tanzania

Vanessa Mdee kuingia studio na rapper Tay Grin wa Malawi

Usiku wa mwaka mpya, Vanessa Mdee alikuwa kwenye stage za Malawi akitumbuiza kama show ya kuingilia mwaka mpya.

Vanessa hakuishia na kutumbuiza tu bali amepata fursa ya kuingia studio na rapper wa Malawi Tay Grin ambaye alikua akitamani sana kufanya collabo na mwanadada huyo wa Cash Madame.
 
Tukiingoja hii collabo, kwa sasa burudika na hit ya Vanessa ya Cash Madame kwenye Mzooka ndani ya Maisha Magic Bongo, Jumatatu hadi Ijumaa saa 16:00.
 
Vanessa na rapper Grin wamepost picha kuonesha kudhihirisha hilo kwenye ukurasa wao wa Instagram wakipiga kazi kwa kupokezana kuingiza sauti yani wakirecord studio session.
 
Rapper Tay alishare picha na kuandika haya kwenye ukurasa wake wa instagram:
“Studio session! @vanessamdee @sonyezo and yours truly. The fire levels on this song is on the higher side. CANT wait for y’all to hear it. Too much."
 
Tukirecall mahojiano na rapper Tay kwa mwaka 2016 hii ndio ilikuwa comment yake kwa wasanii wa Tanzania na jinsi gani alitamanii sana kuingia nao studio na hivi sasa ameanza na Vanessa.

"Napenda jinsi wasanii wa Tanzania wanavyoimba. Ni kimuziki sana hata kama sizungumzii Kiswahili, muziki wao unasikika vizuri na ni mtamu. Nimesikiliza wasanii kama Vanessa Mdee, Diamond Platnumz, Alikiba na muziki wao wa bongo flava. Nadhani Nyau Music inaweza kuchanganyikana vizuri na wasanii hawa wakali. Kwa sasa ninafanyia kazi wimbo na Vanessa Mdee na nina matumani ya kumpata Diamond Platnumz kwenye wimbo huo."